Msanii mpya wa Zanzibar Doz Lee atoa nyimbo mpya Uzuri Wako
Msanii huyo anaishi Mwera, Zanzibar, Tanzania......
Sikiliza na Download Hapa:
Ujuzi Time
Habari Mchanganyiko
Sunday, May 18, 2014
New Track - Doz Lee - Uzuri wako
Friday, May 16, 2014
Dogo Fani - Naumwa Video itatoka Karibu (Coming Soon)
Wimbo mpya wa Dogo Fani (Fani Baby) - Naumwa inataka kutoka Official Video ya Wimbo huo, ambayo inayosubiriwa na washabiki wengi wa Msanii huyo.. Msanii wa Kizazi kipya Zanzibar
Angalia na Download
Angalia Video hiyo wakati unapotayarishwa :
Dogo Fani - Video Making | Youtube
Thursday, May 15, 2014
Serikali ya Tanzania imethibitisha mradi wa Treni za juu kama hizi kujengwa Dar hivi karibuni.

Umekua ni usafiri mwingine mzuri na wenye starehe yake kama ukipata nafasi ya kuutumia kwenye nchi zilizoendelea kama Marekani, Uingereza Dubai na kwengineko ambako kuna watu wengine wanategemea sana kuutumia na kuacha magari yao nyumbani na kujikuta wamewahi town na kumaliza shughuli zao manake hamna foleni.
Dar es salaam likiwa jiji la tisa kwa ukuaji duniani huku kwa Afrika likishika nafasi ya tatu, limekua na foleni kubwa ambazo mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inasema huwa kila siku inapatikana hasara ya shilingi BILIONI TATU kutokana na foleni Dar es salaam.

Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’
Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.
Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni lazima uwepo kwa saa 24′

Kazi hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha Mwanza na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi ya watu elfu moja.
Una imani kwamba hili la treni litafanikiwa Tanzania hivi karibuni? utapendelea kutumia usafiri wa treni? nipe maoni yako kwa kuniandikia hapa chini..
Monday, May 12, 2014
Mchezaji wa NFL Michael Sam Ajitangaza kuwa Shoga

Mchezaji mmoja wa timu ya ligi ya soka ya Marekani, National Footbal League ,Michael Sam amekuwa mchezaji wa kwanza kutangaza wazi kwamba yeye ni shoga katika mchezo huo.
Sam alikuwa ameteuliwa na timu ya Saint Louis Rams katika siku ya mwisho ya usakaji wa vipaji katika mchezo huo ulio maarufu zaidi nchini marekani.
Hatua hiyo ya Michael Sam kutangaza jinsia yake mnamo mwezi february baada ya kukamilisha masomo yake ya mchezo huo katika chuo cha Missouri ilipongezwa ,huku rais Obama akiwa miongoni mwa watu waliotoa pongezi zao.
Baadhi ya wachambuzi wa michezo walikuwa wamebashiri kwamba baadhi ya timu huenda zikajitenga na umaarufu unaomzunguka mchezaji huyo.
Watoto Mapacha wazaliwa wakishikana mikono Marekani

Mama wa mapcha hawa amesema mapacha wake ni zawadi kubwa kwake
Mama mmoja nchini Marekani, amejifungua watoto pacha wakiwa wameshikana mikono.
Watoto hao pia walikuwa wanapumua bila usaidizi wowote walipotolewa kutoka katika mashine yenye hewa ya Oxygen.
Mama wa watoto hao, alisema kuwa watoto hao waliopewa majina ya Jillian na Jenna Thistlewaite walikuwa wameshikana katika kitovu na kutumia Kondo moja la nyuma , hali ambayo madaktari walisema ni nadra.
"Tayari wanaonekana kuwa marafiki ,’’ alisema mama yao Sarah Thistlethwaite.
Walizaliwa Ijumaa katika jimbo la Ohio, wakiwa wameshikana mikono.
Inaarifiwa ni mama mmoja tu kati ya akina mama elfu kumi mwenye uwezo wa kujifungua watoto pacha wa aina hiyo.
Bi Thistlewaite, mwenye umri wa miaka 32,alilazimika kupumzika kwa wiki kadhaa kabla ya kujifungua kwani pacha wanaozaliwa wakiwa wameshikana mikoni ni hali nadra ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya watoto na mama kabla ya kuzaliwa.
Mama huyo alisema kupokea watoto wake ilikuwa zawadi tosha kwake wakati huu wa kusherehekea siku ya akina mama duniani.
Tuesday, May 6, 2014
ACT - TANZANIA Chama kingine cha Siasa Kusajiliwa
CHAMA cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), jana kilikabidhiwa cheti cha usajili wa kudumu na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
Jaji Mutungi alikabidhi cheti hicho mjini Dodoma jana kwa Kaimu Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Kadawi Limbu na kuwataka viongozi wa chama hicho kufanya siasa zenye ukomavu kwa kuzingatia Sheria ya Vyama vya Siasa.
Aliwataka viongozi wa chama hicho, kuheshimu wanachama wao kwani vyama vingi vikishapata usajili, viongozi wake wanaanza kujiona wanajua kuliko wanachama wao.
“Mmepata usajili huku nchi ina amani, fanyeni siasa zitakazohakikisha nchi inaendelea kuwa na amani,” alisema Jaji Mutungi na kutaka chama hicho kushiriki kutoa maoni kuhusu marekebisho Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi.
Msaidizi wa Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, alipongeza ACT kwa kutimiza masharti yote ya kupata usajili wa kudumu na kuongeza kuwa chama hicho kilifanikiwa kupata wanachama zaidi ya 200 katika mikoa 10 ya Tanzania Bara na mikoa miwili kutokea Zanzibar.
Aliwataka viongozi wake kufahamu kwamba sasa wako chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kuwataka kuepuka ushindani na vyama vingine unaoweza kusababisha wasahau sheria zinazoongoza vyama vyao.
“Epukeni kujihusisha katika vurugu, Sheria inakataza vyama vya siasa kutumia nguvu katika siasa, hali hiyo inafifisha demokrasia na kuwatia hofu wanachama,” alisema Nyahoza.
Aliwataka kuepuka migogoro ya ndani ya chama chao kwakuwa mara nyingi vyama vya siasa vinapotafuta, viongozi wake wanakuwa pamoja, wakishapata wengine wanaota mapembe. Limbu alisema chama hicho kimepanga kuonesha demokrasia ya kweli nchini na hakitakuwa chama cha vurugu.
“Chama hiki kitakuwa chama cha heshima, hakitakuwa na mmiliki kitakuwa cha wanachama, hatutegemei migogoro na tutafanya siasa za kistaarabu,” alisema.
Alisema chama hicho kitashiriki kikamilifu kufanyia maboresho Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria Gharama za Uchaguzi, ikiwemo kuhakikisha Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa inakuwa na meno kwa vyama vya siasa,” alisema Limbu.
Kuhusu chama hicho kuwa na watu maarufu nyuma yake, Limbu alisema hayo ni masuala ya kusikika sio kweli kwani wao ni wanasiasa wazoefu, wanajiamini na hakuna sababu ya kufanya kazi kwa kuwa kuna watu nyuma yao.
“Kuna watu na viongozi wa vyama vingine wanakerwa na demokrasia ndani ya vyama vyao, vipo vyama ambavyo ni kampuni ya watu, ukionekana kugusa maslahi ya mtu unafukuzwa tunawakaribisha waje tujenge demokrasia ya kweli,” alisema Limbu.
Monday, May 5, 2014
Channel Bora za Movie Azam Tv
Katika Decorder ya Azam Tv kuna Channel Nzuri nyingi lakini hapa nitaziweka Best for Movies
Movie za Kizungu:
1. MBC2 : MBC 2 Ni Channel bora kwa michezo ya Kizungu (USA, UK) na nchi nyengine zilizoendelea
Bollywood (Movie za Kihindi)
1.Zee Cinema: Zee Cinema ndio Tv bora kwa michezo ya Bollywood ambayo wanaleta michezo mikali ya MaStar wakubwa wa Boolywood.
2. Star Gold: Star Gold ni TV inayopendwa sana na wao vile vile wanaleta Movie kali za Super Star wakubwa wa Bollywood
3. Sinema Zetu: Najua WaTanzania tunapenda sana filamu zetu za Tanzania kwa Sababu ya Lugha tunayoifahamu fasaha, Sinema zetu inaweka michezo ya Bongo tu (Filamu za Kiswahili) massa 24.